Mara baada ya Willian kushinda tunzo hiyo, kinda wa Chelsea, Callum Hudson Odoi naye amechaguliwa kuwa mshindi wa tunzo ya mchezaji bora wa mwezi Januari kwa ligi kuu ya vijana inayotambulika kwa jina la Premier League 2 ambapo akishinda tunzo hiyo kwa kucheza mchezo mmoja tu, na kwa kiwango alichokionyesha kwenye mchezo huo huku akifunga magoli matatu kimemfana kushinda tunzo hiyo.
Kinda huyo mwenye miaka 17 kwa sasa, ameshinda tunzo yake hiyo huku akiendeleza umwamba wake akionekana kuwa mmoja wa nyota watakaokuja kuvuma sana miaka ya karibuni kutokana pia na kupata nafasi ya kucheza kwenye timu ya wakubwa na kucheza michewzo kadhaa ya ligi kuu.
Nyota huyo alipohojiwa kuhusu tunzo hiyo alisema "Ulikuwa ni mwezi wangu bora na ni ngumu kuamini. Nilipofunga magoli matatu dhidi ya Sunderland na kupata habari kuwa nimechaguliwa kuwa kwenye benchi la timu ya wakubwa itakayocheza dhidi ya Newcastle katika mchezo wa FA, lilikuwa jambo kubwa na muhimu kwangu" alisema kinda huyo.
No comments:
Post a Comment