Nyota wa klabu ya Chelsea ambaye ni raia wa Ubelgiji, Eden Hazard amekuwa akihusishwa kwa muda kutakiwa na klabu inayoshiriki ligi kuu nchini Hispania kwa muda mrefu na ilionekana kukaribia kujiunga kwenye klabu hiyo kabla ya nyota huyo kupata majeruhi yaliyomweka nje kwa muda mrefu.
Lakini sasa nyota huyo mwenye miaka 27 kwa sasa anatajwa kwa karibu kutimkia kwenye klabu hiyo mara baada ya kutoka taarifa zikimhusisha nyota huyo kutafuta nyumba kwenye jiji la Madrid, inapopatikana klabu hiyo nchini Hispania ambapo inaelezwa kuwa nyota huyo anataka kujiunga na klabu hiyo ili kupata changamoto mpya na kushinda mataji mengine tofauti ikiwemo taji la ballon d'or ambayo inaonekana ni ngumu kushinda kama ataendelea kubaki Uingereza.
Ila fununu hizi zimezuka mara baada ya nyota huyo kutoa kauli mara baada ya kuiongoza vyema Chelsea kupata ushindi wake katika mchezo wa 27 wa ligi kuu Uingereza.
"Timu inatakiwa imalize kwenye nafasi nne za juu katika msimamo wa ligi kuu, ili tuweze kucheza michuano ya klabu bingwa msimu ujao. Msimu huu tunashiriki michuano kadhaa na itakuwa vyema kama tukibeba kombe la FA, lakini ni ngumu sana kushinda klabu bingwa lakini ni vyema kama tukipambana zaidi kuendelea kuwepo kwenye michuano hiyo" kwa kauli hiyo ya kuonekana kutamani kwake kucheza michuano ya klabu bingwa, imetazamiwa kama kutamani kwake kucheza kwenye klabu itakayokuwa kwenye michuano ya klabu bingwa, na kuonekana itakuwa ngumu kwa Chelsea kuendelea kubaki nae kama itashindwa kufudhu kucheza michuano hiyo msimu ujao.
No comments:
Post a Comment