Chelsea itacheza dhidi ya Hull city siku ya ijumaa katika michuano ya kombe la FA, ambapo mchezo huo utachezwa kwenye uwanja wa Chelsea, Stamford Bridge. Kuelekea kwenye mchezo huo, uongozi wa Chelsea umetoa taarifa mpya kabla ya kumenyana na klabu hiyo inayoizidi Chelsea kwa mwaka mmoja katika kuundwa kwake. Hull city iliundwa mwaka 1904 wakati Chelsea ilizaliwa siku ya tarehe 10-Marchi-1905.
Uongozi wa Chelsea umegoma kuwaruhusu wachezaji wake Fikayo Tomori na Ola Aina ambao wanaichezea kwa mkopo klabu hiyo ya Hull city kucheza siku hiyo ya ijumaa usiku.
Tomori na Aina ambao wanacheza kwenye klabu hiyo inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Uingereza maarufu kama Championship hawatoruhusiwa kucheza katika mchezo huo kutokana na kuhesabika kama wachezaji wa Chelsea kama sheria za uhamisho zinavyosema.
Sheria za uhamisho zinampa rungu mmiliki wa mchezaji kuamua kama mchezaji wake aliyepo kwa mkopo kwenye klabu nyengine anaruhusiwa kucheza pindi klabu hizo zinapomenyana au haruhusiwi kutokana na nyota huyo kuhesabika kama mchezaji wa timu nyengine kwa mfano hapa tunaiangalia Chelsea na wachezaji wake Ola Aina na Fokoyi Tomori, nyota hao wanalipwa na Chelsea kutokana na kumilikiwa na klabu hiyo na ndio maana klabu inapewa rungu hilo.
No comments:
Post a Comment