Monchi alipohojiwa alisema "Mazungumzo kati ya Chelsea na Roma yalikuwa juu ya kumsajili mlinzi Emerson Palmieri (ambaye kwa sasa ni mchezaji wa Chelsea) lakini baadae Dzeko akaingia katikati ya mazungumzo wakimtaka nayeye. Si jambo zuri kumuuza mchezaji wako nyota, lakini inategemea ni ofa gani imewekwa mezani ili kumsajili"
"Tulichoshindwana na Chelsea ni katika mahitaji ya klabu, ambapo hawakuwa tayari kufata mahitaji tunayotaka. Tulishakuwa tayari na nia ya kuwasajili washambuliaji wengine ili kuziba pengo la Dzeko klabuni, Olivier Giroud na Michy Batshuayi walikuwa kwenye mipango ya klabu kama Dzeko angeondoka basi wao wangechukua nafasi yake" alisema kiongozi huyo.
Chelsea ilikamilisha usajili wa mchezaji raia wa Ufaransa, Olivier Giroud aliyesajiliwa akitokea klabu ya Arsenyani (Arsenal) kwa dau la paundi milioni 18 (Shilingi za Tanzania bilioni 57) huku kwa Michy Batshuayi akitolewa kwa mkopo na kujiunga na klabu ya Borrusia Dortmund ambapo atakuwa huko mpaka mwisho wa msimu.
No comments:
Post a Comment