Kocha wa zamaniwa klabu ya Barcelona, Luis Enrique ambaye amekuwa akihusishwa kuwa mrithi wa Antonio Conte labuni Chelsea, anaweza asijiunge na klabu yoyote kutokana na makocha wake wasaidizi kumgomea kujiunga nae endapo akijiunga na Chelsea au hata Arsenyani (Arsenal) ambao nao wanamtaka ili awe mrithi wa Arsene Wenger klabuni hapo.
Taarifa zinasema makocha wake wasaidizi ambaye mmojawapo ni Juan Carlos Unzue wanaoifundisha klabu ya Celta Vigo ya nchini Hispania, hawataki kuungana na kocha huyo na badala yake wanataka kuendelea kubaki kuwa klabuni hapo.
Juan Carlos Unzue ndiye alikuwa kocha msaidizi wake pindi walipokuwa wote klabuni Barcelona, lakini mara baada ya kocha huyo kuachana na wababe hao wa Hispania akaamua kupumzika, wakati akiwa mapumzikoni kocha huyo Unzue pamoja na makocha wengine wa benchi la ufundi lililokuwa chini ya Enrique wakapata kibarua kwenye klabu ya Celta Vigo, na sasa wanatumia majukumu huko na hawapendezwi na kuungana na kocha wao huyo.
Kwa maana hiyo, kama kocha Enrique atatua Chelsea au klabu nyengine atatakiwa kuunda upya benchi lake la ufundi ili kuliendeleza gurudumu.
MPANGO WA ENRIQUE KUJIUNGA NA CHELSEA WAINGIA DOA
Share This
Tags
# Chelsea Usajili
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Usajili
Labels:
Chelsea Usajili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment