Katika mchezo huo, kulitokea tukio moja ambalo liliwahuzunisha wengi japo halikuonekana kama tukio kubwa sana maana halikuonekana kama lilileta madhara makubwa mpaka hivi leo nyota huyo anayeitwa Ryan Mason anapotangaza kustaafu sok mara baada ya kufanyiwa upasuaji na kuonekana itakuwa ni hatari kwake kuendelea kucheza soka.
Ryan ametangaza kustaafu kucheza soka akiwa na miaka 26 mara baada ya kufanyiwa upasuaji toka mwezi Januari-2017 mpaka hii leo anakuja kutangaza kustaafu akiwa ndio kwanza ana umri mdogo.
Ripoti iliyotolewa na klabu yake inaeleza kuwa kutokana na kufanyika uchunguzi wa kitabibu haijashauriwa nyota huyo aliyekuwa na uwezo mkubwa kucheza kama kiungo kuweza kuendelea na soka na badala yake analazimika kustaafu kucheza mchezo huo na nyota huyo anapenda kusema asante na kutoa shukrani kwa kila aliyehusika kwenye matibabu yake mpaka leo kuwa mzima.
Chelsea itapambana na klabu hiyo ya Hull city ijumaa hii katika michuano ya kombe la FA ambapo Chelsea itakuwa nyumbani Stamford Bridge na huenda Ryan akawepo uwanjani kupokea heshima maalumu.
No comments:
Post a Comment