Jana kwenye mchezo wa Chelsea dhidi ya West Bromwich kuna tukio huenda hukuliona, na hata kama uliliona naamini hukujua kilichoendelea ni nini maana ni kama hakikuwa na mwendelezo. Jana katika mchezo huo ambao Chelsea ilicheza dhidi ya West Bromwich na ushindi mnono wa mabao 3-0, kuna mtoto mmoja alionyesha bango akimuomba mchezaji wa Chelsea, Cesar Azpilicueta.
Ilikuwa ivi kijana huyo aliandika kwenye aina flani hivi ya bango likisomeka "Jana wakati nacheza mpira kidole gumba changu kilivunjika. Siwezi kucheza mpira kwa wiki nne, je unaweza kunisaidia kwa kunipa jezi yako? Na je kuna uwezekano wa kunisainia? Naitwa Reggie nina miaka 7"
Ujumbe huo ni kama haukuonekana, lakini Cesar Azpilicueta mwenyewe ambaye ni nahodha msaidizi wa Chelsea aliuona ujumbe huo na kupitia mtandao wa Twitter akamjibu kijana huyo kwa kuandika "Hello Reggie, iambie familia yako ifanye mawasiliano na mimi na nitakuwa mwenye furaha kwa kukutumia jezi iliyosainiwa. Uwe mwangalifu #BlueFamily"
Hii inakuwa ni mfululizo wa matukio kwa wachezaji wa Chelsea kuombwa jezi na mashabiki ambapo kama unakumbuka vizuri ilishatokea kwa Eden Hazard katika mchezo dhidi ya Brighton ambapo Eden Hazard aliombwa jezi na kumpatia mtoto huyo.
Je kama ndio leo ukipata nafasi ya kukutana na wachezaji wa Chelsea, ni mchezaji gani ungemuomba?
AZPILICUETA NAYE NI KAMA HAZARD
Share This
Tags
# Chelsea Habari
# Mitandaoni
Share This
About Darajani 1905
Mitandaoni
Labels:
Chelsea Habari,
Mitandaoni
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment