KYLE SCOTT NI NANI? - Darajani 1905
Katika mchezo wa jana ambao Chelsea ilimenyana dhidi ya Hull city katika haua ya 16 bora ya michuano ya kombe la FA ambapo Chelsea ilijipatia ushindi wa mabao 4-0, kuna wachezaji wengi waliweka historia mara baada ya kucheza michezo yao ya kwanza klabuni Chelsea kwenye kikosi cha wakubwa. Trevoh Chalobah ambaye ni nyota wa kikosi cha Chelsea cha akademi alikuwa katika kikosi cha wakubwa kwa mara ya kwanza tangu atue Chelsea kama haujui huyu ndiye mdogo wa kiungo wa zamani wa Chelsea, Nathan Chalobah ambaye aliuzwa na kujiunga na klabu ya Watford katika dirisha kubwa la usajili lililopita. Lakini mwengine ani Kyle Scott, ambaye huyu aliweka historia ya kucheza mchezo wake wa kwanza wa kimashindano kwa Chelsea, alipoingia kuchukua nafasi ya Cesc Fabregas katika dakika ya 62 ya mchezo huo.

Sasa hapa nataka nikuletee makala juu ya nyota huyu, Kyle Scott ambaye alionekana kuwa nyota wa baadae mara baada ya kuonyesha ubunifu mkubwa kwenye nafasi ya kiungo akileta uwiano mzuri katika nafasi ya kiungo akiwa sambamba na Danny Drinkwater.

Kyle Scott ni nani?
Kyle Scott ni kijana raia wa Marekani aliyewai pia kuichezea timu ya taifa ya Uingereza kwa upande wa vijana na alizaliwa tarehe 22-Desemba-1997 ambapo pia ana asili ya jamhuri ya Ireland.


Ana historia gani ndani ya Chelsea?
Kiungo huyu alifika Chelsea akiwa na miaka 10 akitokea kwenye akademi ya Southampton, na alicheza hapo kwa muda mrefu na alihusika kwenye kikosi cha vijana kilichobeba mataji sita kwa misimu mitatu wakibeba kombe la FA kwa misimu mitatu mfululizo yaani 2013-2014, 2014-2015, 2015-2016 huku pia akiisaidia kubeba kombe la klabu bingwa Ulaya kwa vijana maarufu kama UEFA Youth League kwa misimu miwili mfululizo yaani 2014-2015 na 2015-2016.


Aliwai kutaka kujiunga na klabu ya Willem II ya nchini Uholanzi mara baada ya kuona nafasi ya kucheza timu ya wakubwa ni ngumu ambapo alienda huko mwaka 2016 kwa ajili ya majaribio akiomba kutolewa kwa mkopo kabla ya mpango huo kuvunjika na kurudi Chelsea.

Bahati ikamdondokea kwenye kikosi cha Antonio Conte
Chini ya kocha Antonio Conte, nyota huyo akaanza kupata mfululizo wa bahati mara baada ya kupambana kwa muda mrefu, ndipo akaanza kuona matunda ya uvumilivu mara baada ya kuchaguliwa kwenye kikosi cha Chelsea kilichosafiri kwenda kwenye michezo ya kirafiki kujiandaa na msimu mpya kwa mwaka 2017, ambapo aliuhisika kwenye mchezo ambao Chelsea ilimenyana na Arsenyani (Arsenal) huko nchini Indonesia na Chelsea kupata ushindi wa mabao 3-0.


Lakini pia jambo kubwa kwake na huenda likamfanya ajione sasa kuwa ana upekee ni pale alipochaguliwa kwenye kikosi cha Chelsea kitakachoshiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya kwa msimu huu akiwa ni mmoja wa wachezaji wachache waliotoka kwenye kikosi cha vijana kuchaguliwa kwenye kikosi hicho na anaweza akatumika kuanzia kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora ambapo Chelsea itamenyana dhidi ya Barcelona. Wachezaji waliochaguliwa ni Willy Caballero, Thibaut Courtois, Eduardo, Antonio Rudiger, Marcos Alonso, Davide Zappacosta, Gary Cahill, Andreas Christensen, Cesar Azpilicueta, David Luiz, Emerson Palmieri, Dujon Sterling, Cesc Fabregas, Danny Drinkwater, N'Golo Kante, Ross Barkley, Eden Hazard, Pedro, Tiemoue Bakayoko, Victor Moses, Willian, Kyle Scott*, Alvaro Morata, Olivier Giroud, Callum Hudson-Odoi.

Lakini kama hilo halitoshi, nyota huyo kuichezea Chelsea mchezo wa kimashindano kwa mara ya kwanza huku nyota huyo akiingia kama mhezaji wa akiba kuchukua nafasi ya Cesc Fabregas hapo jana.

Aina yake ya uchezaji
Kyle Scott anatajwa kuwa mmoja wa makinda wenye uwezo mkubwa wa kucheza kama kiungo cha kati, lakini pia akiwa na uwezo mkubwa wa kuzuia mashambulizi kwa nguvu (Hard-tackling Midfilder) huku  akiwa na uwezo mkubwa wa kutulia na mpira na kuchezesha timu kama kazi ya kiungo inavyotakiwa.

Usilolijua kuhusu Scott
Kyle Scott katika mchezo huo wa jana, alikuwa ndiye mmarekani wa tatu kuwai kuichezea Chelsea tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo mwaka 1905, waliomtangulia ni pamoja na Matt Miazga ambaye kwa sasa anaichezea kwa mkopo klabu ya Vittese ya nchini Uholanzi pamoja na Roy Wagergle.

No comments:

Post a Comment