FA; CHELSEA 4-0 HULL CITY-WILLIAN APIGA MBILI, GIROUD AANZA NA MOTO - Darajani 1905

FA; CHELSEA 4-0 HULL CITY-WILLIAN APIGA MBILI, GIROUD AANZA NA MOTO

Share This
Chelsea inapata ushindi wake muhimu katika uwanja wake wa nyumbani katika michuano ya kombe la FA ikiibamiza Hull city kwa magoli 4-0 na hivyo kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
Chelsea imepata ushindi huo mnono magoli yake yakifungwa na Willian aliyefunga mara mbili ambaye alichaguliwa pia kuwa nyota wa mchezo na jengine likifungwa na Pedro huku na jengine likifungwa na mshambuliaji mpya wa Chelsea, Olivier Giroud akipokea pasi murua iliyotoka kwa mlinzi Emerson Palmieri ambaye naye ni mpya klabuni hapo na ndio alikuwa akicheza mchezo wake wa kwanza.
Mpira ulianza, na katika dakika ya  kwanza tu, zilimtosha Willian kufunga goli hilo kabla ya Pedro kufunga tena jengine akipokea pasi kali iliyopigwa na Cesc Fabregas huku jengine likifungwa na Willian akipokea pasi ya Giroud aliyetumia ubavu vyema kumnyang'anya mpira mlinzi wa Hull city huku Giroud akifunga goli lake muhimu na la kwanza tangu atue Chelsea katika dirisha dogo la usajili.
Baadhi ya rekodi zilizowekwa;
-Mpaka sasa ndani ya msimu huu, Chelsea imeshuhudia wachezaji wake 18 tofauti wakiifungia klabu hiyo katika michuano yote, ni msimu wa 2005-2006 tu ulishuhudia wachezaji wengi. Wachezaji 20.
-Mwaka 2015, ndio ulikuwa mwaka wa mwisho kwa Chelsea kufunga magoli 4 katika kipindi cha kwanza kabla ya leo kufanya tena ivo.
-Kyle Scott ambaye ameichezea Chelsea leo mchezo wake wa kwanza akiingia kuchukua nafasi ya Cesc Fabregas amekuwa mmarekani watatu kuichezea Chelsea. Lakini pia amekuwa mchezaji wa 737 kuichezea Chelsea. Wamarekani wengine kuichezea Chelsea ni Matt Miazga na Roy Wagergle.
-Emerson Palmieri amekuwa mchezaji wa 736 kuichezea Chelsea toka kuanzishwa kwake mwaka 1905.
-Mpaka sasa Willian Borges amefikisha magoli 40, magoli yanayomfanya kumfikia Gianluca Vialli huku akiwaacha Joe Cole.

No comments:

Post a Comment