NYOTA WA CHELSEA AWEKA REKODI, ATOA UJUMBE MZITO - Darajani 1905

NYOTA WA CHELSEA AWEKA REKODI, ATOA UJUMBE MZITO

Share This
Nyota wa Chelsea, Trevoh Chalobah ambaye jana alihusika kwenye kikosi cha Chelsea kwa mara ya kwanza ambapo Chelsea ilikuwa uwanjani kupambana dhidi ya Hull city kwenye mchezo ulioisha kwa Chelsea kupata ushindi wa mabao 4-0 na kufanikiwa kufudhu kucheza hatua ya roobo fainali ya michuano hiyo.

Hiyo ni rekodi na mwanzo mzuri kwa nyota huyo ambaye amecheza kwa mafanikio kwenye kikosi cha Chelsea ya vijana akicheza nafasi ya ulinzi wa kati na ina dalili nzuri kwake kuwa ana nafasi kubwa ya kufanya makubwa kwenye kikosi cha Chelsea. Kupitia mtandao wa Twitter, nyota huyo ametuma ujumbe kumuonyesha bado hajakata tamaa na anaendela kupambana licha ya kutopata nafasi katika mchezo wa jana. Lakini ujumbe huu ni muhimu kwa kila anayetamani kufanikiwa kwenye maisha ya hapa duniani nikiwemo nami mwandishi pia.

Kupitia mtandao huo, alituma picha inayoeleza "New York (jiji la nchini Marekani) lipo mbele masaa matatu zaidi ya Calfornia (jiji jengine la Marekani) lakini kwa maana hiyo haifanyi maendeleo yake kuwa ya taratibu. Kuna mtu anahitimu masomo yake akiwa na miaka 22, lakini anapata kazi nzuri mara baada ya kusubiri kwa miaka mitano. Kuna mwengine amekuwa mmiliki wa kampuni fulani akiwa na miaka 25 lakini akafariki akiwa na miaka 50, wakati mwengine amekuwa mmiliki wa kampuni akiwa na miaka 50 lakini akaishi mpaka kufikia miaka 90. Kuna mtu hana mahusiano ya kimapenzi, wakati kuna mwengine ameoa. Barrack Obama alistaafu urais akiwa na miaka 55 wakati Donald Trump amekuwa rais akiwa na miaka 70. Kila mmoja anaishi kupambana na muda wake, inawezekana waliokuzunguka wapo mbele ya uda wako na wengine wakiwa nyuma ya muda wako. Lakini kila mmoja anapambana katika maisha yake, na katika muda wake. Usiwalaumu wala kuwanyooshea kidole. Wao wapo kwenye muda wao wakati na wewe unaishi kwenye muda wako. Maisha ni kusubiri muda wako ufike nawe ndipo uingie kupambana.
Kwa hiyo, tulia.
Haujachelewa, na wala haujawai.
Upo sawa na muda wako."

Nyota huyo alizaliwa tarehe 5-Julai-1999, na kama haujui ni mdogo wa kiungo wa zamani wa Chelsea, Nathan Chalobah ambaye aliuzwa kujiunga na watford kwenye dirisha la usajili.

No comments:

Post a Comment