MORATA NA MKEWE WAZUA MASWALI MENGI KWA CONTE - Darajani 1905

MORATA NA MKEWE WAZUA MASWALI MENGI KWA CONTE

Share This
Kocha Antonio Conte siku ya jumanne alifanya mkutano na waandishi wa habari katika kujiandaa na mchezo wa ligi kuu unaochezwa leo jumatatu usiku ambapo Chelsea itakuwa nyumbani kupambana dhidi ya West Bromwich ambapo katika mchezo wa kwanza wa mzunguko wa kwanza, Chelsea ilishinda kwa mabao 4-0.
Siku hiyo Conte aliulizwa swali na waandishi hao wa habari juu ya matokeo mabaya ambayo Chelsea imefululiza kuyapata katika michezo miwili ya mwisho dhidi ya Afc Bournemouth na Watford, na kocha huyo kusema haina haja sana ya kuzungumzia matokeo mabovu wakati timu inawakosa wachezaji wake wa umuhimu kama Alvaro Morata ambaye majeruhi yake ya mgongo yanamfanya kukaa nje kwa muda usiojulikana lakini inaweza kumgharimu mpaka kukaa nje msimu mzima.
Lakini katika siku hizi mbili zilizopita, yaani jumamosi ya juzi na jumapili ya jana kumezuka sintofahamu juu ya mchezaji huyo raia wa Hispania ambaye aliigharimu Chelsea paundi milioni 60 kutoka Real Madrid na kutua hapo ambapo Chelsea ilikamilisha usajili wake muda mfupi mara baada ya kumuuza mshambuliaji wake aliyeisaidia kutwaa taji la ligi kuu msimu uliopita, Diego Costa ambaye aliuzwa kwenda Atletico Madrid kwa dau la paundi milioni 57.
Muda mfupi mara baada ya kocha Antonio Conte kusema ivo juu ya wasiwasi wa kukaa nje kwa Alvaro Morata, nyota huyo alipiga picha na kutuma ujumbe katika mtandao wa Twitter akionekana kuwa kwenye gari pamoja na nyota mwengine wa Chelsea, Davide Zappacosta na mshambuliaji huyo kuandika "Nimetoka mazoezini, na sasa nipo njiani kurudi nyumbani" ambapo taarifa hiyo ilikuwa tofauti na alichokisema Antonio Conte kuhusu mchezaji huyo.
Lakini tena, jana kupitia mtandao wa Instagram, mke wa mchezaji huyo, Alice Campelo alituma video katika mtandao wa Instagram, ikimuonyesha akiwa na Morata wakiwa wanacheza na nyota huyo kuonekana akiwa amembeba kabisa mke wake huyo huku ikiwashangaza watu maana hakuonekana akiwa na matatizo ya mgongo kabisa. Sio kama ilivyokuwa inaripotiwa na kocha Antonio Conte.
Labda kwa kuwa Antonio Conte, kwa alivyoripoti hakuwa na taarifa zaidi juu ya mchezaji huyo na ndio maana alisema hajui nyota huyo atakaa nje kwa muda gani iwe kwa siku moja, siku mbili, mwezi au hata msimu mzima.
Bado kuna maswali mengi katika hili, maana kwa kawaida, kocha ndiye msimamizi wa mchezaji maana kila mchezaji yupo chini yake na yeye ndiye anapaswa kujua kinachoendelea kwa mchezaji wake. Huenda kuna kutokuelewana kati ya wachezaji na kocha, huenda kuna mgogoro unaoendelea chini kwa chini juu ya kocha Antonio Conte haswa kama ilivyowai kuripotiwa na mwandishi mmoja wa chombo cha habari cha ESPN cha nchini Brazil kuwa Antonio Conte mpaka sasa anapata mchango wake wa moja kwa moja kutoka kwa Cesar Azpilicueta tu, ila wachezaji wengine wanaonekana kumtenga. Kuisoma taarifa hiyo bonyeza hapa



No comments:

Post a Comment