KOCHA WA WEST BROM AMUONGELEA COSTA KUELEKEA LEO USIKU - Darajani 1905

KOCHA WA WEST BROM AMUONGELEA COSTA KUELEKEA LEO USIKU

Share This
Chelsea leo itakuwa nyumbani kucheza dhidi ya klabu ya West Bromwich maarufu pia kama The Baggies, ambapo mchezo huo utakuwa wa raundi ya 27 ya ligi kuu Uingereza kwa msimu wa 2017-2018.

Chelsea itahitaji ushindi wa hali na mali katika mchezo huu ili ijiweke sawa katika msimamo wa ligi kuu Uingereza ambapo kwa sasa inashika nafasi ya tano ikiwa imeachwa alama 2 na Tottenham iliyowafunga Arsenyani (Arsenal) hapo jumamosi, na kama ikifanikiwa kushinda mchezo wa leo itafanikiwa pia kupanda mpaka nafasi ya nne huku ikipishana kwa idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa na Livepumba (Liverpool) ambao wao wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Kuelekea katika mchezo huo, kocha wa klabu ya West Bromwich, Alan Pardew ametoa neno juu ya kocha wa Chelsea, Antonio Conte akisema "Amefanya makubwa hapa Uingereza, katika msimu wake wa kwanza aliifanya timu kuwa imara na yenye ubora. Anastahili sifa katika hilo.".

"Aliifanya Chelsea kuwa klabu bora na ngumu na kutupa uzito katika kufikiri ni kwa jinsi gani tunaweza kuizuia haswa akiwa na kikosi bora. Tunapomuongelea kwa sasa tusisahau hilo" alisema kocha huyo ambaye amewai kuzifundisha klabu za Newcastle, Crystal Palace na sasa West Bromwich.

Na alipoulizwa juu ya Chelsea kwa sasa, alisema "Chelsea ya msimu uliopita ilikuwa ngumu maana ilikuwa na wachezaji imara na wenye uwezo mkubwa. Haswa katika safu ya ushambuliaji, kumkosa Diego Costa ni tatizo sana kwa Chelsea"

"Ni mchezaji mwenye nguvu na mwenye uwezo wa kusababisha madhara kwenye timu yako muda wowote awapo uwanjani. Hata kama sio kwa kufunga, lakini atasababisha madhara makubwa kwa walinzi. Conte anamkosa mchezaji wa aina hiyo"

No comments:

Post a Comment