Michuano ya klabu bingwa Ulaya kwa mwaka 2018 kwa hatua ya 16 bora ishafungua pazia na kwa sasa ni kama ipo sebuleni, ambapo mpaka sasa ishachezwa michezo minne kabla ya michezo mingine minne kumaliziwa wiki ijayo. Kati ya hiyo michezo minne ya wiki ijayo, mchezo utakaotolewa macho na kuangaliwa sana utakuwa ni mchezo wa Chelsea dhidi ya Barcelona, mchezo utakaochezwa tarehe 20-Februari wakati ule wa marudiano utachezwa uko nchini Hispania tarehe 14-Marchi, na tayari tiketi za mchezo huo zishaanza kuuzwa.
Kuelekea kwenye mchezo huo ambapo Chelsea itakuwa nyumbani, mchezaji mpya wa klabu ya Barcelona, Phillipe Coutinho ameitahadharisha klabu yake hiyo juu ya ubora wa Chelsea kuelekea kwenye mchezo huo.
"Chelsea ni timu bora, inayoundwa na washambuliaji hatari, haswa kwenye safu ya ushambuliaji. Wapo vizuri pia kwa mashambulizi ya kushtukiza" alisema nyota huyo raia wa Brazil.
Coutinho alijiunga na klabu hiyo katika dirisha dogo la usajili akitokea Liverpumba (Liverpool) ya nchini Uingereza ambako huko amekuwa akicheza dhidi ya Chelsea kwa maana hiyo anaifahamu vizuri Chelsea. Lakini nyota huyo hatoruhusiwa kuichezea Barcelona katika michuano hii kwa msimu huu kutokana na kuichezea tayari Liverpumba inayoshiriki pia michuano hii.
No comments:
Post a Comment