NYOTA WA MADRID KUTUMIKA KUMVUTA HAZARD - Darajani 1905

NYOTA WA MADRID KUTUMIKA KUMVUTA HAZARD

Share This
Klabu ya Real Madrid imekuwa ikimfukuzia nyota wa Chelsea, Eden Hazard mara kwa mara huku jitihada zao zikigonga mwamba wakishindwa kumnasa nyota huyo mara kwa mara huku wakijaribu kuwatumia nyota wake kama Gareth Bale na hata Marco Asensio kama mabadilishano ili waweze kumnasa nyota huyo lakini mara zote mipango yao imekuwa ikigoma.

Chanzo cha kuaminika kinadai kuwa nyota wa klabu hiyo, Marco Asensio ameongea na kiongozi wa klabu hiyo akisema yupo tayari yeye atumike kama mabadilishano ili aje Chelsea wakati Hazard akijiunga na Real Madrid katika dirisha hili la usajili la kipindi cha kiangazi.

Hazard amekataa mara kwa mara kusaini mkataba mpya klabuni Chelsea licha ya uongozi wa Chelsea kufanya nae mazungumzo ili asaini mkataba mpya na hiyo inatajwa na baba yake, Thierry Hazard kuwa nyota huyo anatamani kucheza Real Madrid na ndio sababu inayomfanya akatae kusaini mkataba wa kuendelea kusalia London.

Mpango huo unaonekana kupata baraka kutoka kwa mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich ambaye anatajwa kuukubali usajili huo wa Marco Asensio kutua Chelsea kisha Hazard aende Madrid mara baada ya washauri wake kumshauri kuwa Asensio ana muda mrefu wa kucheza kuliko Cristiano Ronaldo ambaye mwazoni ilikuwa akitajwa kutumika kama mabadilishano ya usajili huo, na sasa kuna taarifa zinadai kuwa Roman yupo tayari kumpokea Asensio. Asensio kwa sasa ana miaka 22 huku Ronaldo akiwa na miaka 32 wakati kwa Hazard ana miaka 27.

No comments:

Post a Comment