ZAPPACOSTA ATOA NENO KUMHUSU CONTE - Darajani 1905

ZAPPACOSTA ATOA NENO KUMHUSU CONTE

Share This
Mara baada ya kuhusishwa kuondoka klabuni Chelsea ifikapo mwisho wa msimu huu, kocha Antonio Conte jana alikana tuhuma hizo na kukiri anatamani kubaki klabuni Chelsea na hatazamii kuungana na timu ya taifa ya Italia ambapo tetesi na magazeti mengi ya limhusisha kocha huyo kutaka kuondoka klabuni hapo.

Nyota wa Chelsea, davide Zappacosta ametoa neno juu ya kocha huyo na jinsi anavyomchukulia, "Ni kocha bora na aliyekamilika anayeweza kumsaidia mchezaji kuwa sawa kifikra na hata kimawazo. Ni kocha anayeweza kukuambia na kuwa karibu na wewe na kukupa siri juu ya uchezaji wako na nini ukifanye kuwa bora kwa nafasi unayocheza."

"Kwa upande wangu namchukulia ni mmoja ya makocha waliokamilika kwa sifa zote anazopaswa kuwa nazo kocha bora" alisema winga huyo raia wa Italia.

Zappacosta alitua klabuni Chelsea katika dirisha kubwa la usajili akitokea klabu ya Torino na amekuwa akitumika kama mbadala wa Victor Moses kwa nafasi ya winga wa kulia.

No comments:

Post a Comment