WACHEZAJI WA CHELSEA WAWASHA MOTO UKO WALIPO - Darajani 1905

WACHEZAJI WA CHELSEA WAWASHA MOTO UKO WALIPO

Share This
Jana klabu ya Vittese inayoshiriki ligi kuu nchini Uholanzi ilipata ushindi wa magoli 2-0 ilipomenyana dhidi ya Groningen katika mchezo wa ligi kuu nchini humo maarufu kama Eredivisie. Lakini kubwa ni nyota wa Chelsea walioko kwa mkopo kwenye klabu hiyo ya Vitesse kuonyesha kiwango cha juu kwenye klabu hio wakiipatia ushindi klabu hiyo.

matt Miazga alikuwa wa kwanza kuifungia goli la kwanza klabu hiyo inayoshika nafasi ya sita katika ligi hiyo huku Mason Mount akifunga goli la pili ambapo wachezaji hao wote ni wachezaji wa Chelsea na wapo hapo kwa mkopo.

Matt Miazga alitua Chelsea mwaka 2016 na kuichezea michezo miwili tu kabla ya kutolewa kwa mkopo kwenye klabu hiyo ya Vitesse wakati kwa Mason Mount alisajiliwa mwaka 2017 na kutolewa kwa mkopo kujiunga kwenye klabu hiyo.
Lakini mchezaji mwengine wa Chelsea ambaye yeye anaichezea klabu ya Borrusia Dortmund, Michy Batshuayi naye jana aliwasha moto klabuni huko akicheza mchezo wake wa kwanza tangu ajiunge nayo kwa mkopo akiifungia magoli mawili na kutengeneza jengine moja na kuifanya klabu hiyo ipate ushindi mzuri ugenini wa magoli 2-3 dhidi ya FC Koln.
Ila pia nyota mwengine wa Chelsea aliyekwamkopo kwenye klabu ya Birmingham inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Uingereza, Jeremie Boga aliipatia ushindi klabu yake hiyo akiifungia goli moja katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Sunderland ambayo inachezewa na nyota mwengine wa Chelsea Jean Clarke Salter ambaye naye yupo uko kwa mkopo. Mchezo huo ulichezwa tarehe 30-januari mwaka huu.

No comments:

Post a Comment