BATSHUAYI AANZA NA MOTO DORTMUND - Darajani 1905

BATSHUAYI AANZA NA MOTO DORTMUND

Share This
Nyota mpya wa klabu ya Borrusia Dortmund, Michy Batshuayi ameanza na moto wa hali ya juu klabuni hapo mara baada ya kuiongoza vyema kupata ushindi muhimu wa mchezo wa ligi kuu Ujerumani maarufu kama Bundesliga.

Batshuayi ambaye ni mchezaji wa Chelsea ingawa yupo hapo kama mchezaji wa mkopo, jana aliipatia ushindi muhimu klabu yake hiyo akifunga magoli mawili katika mchezo wake wa kwanza toka ajiunge na klabu hiyo siku ya mwisho ya dirisha la usajili ambapo jana aliichezea mchezo wake wa kwanza na kuipatia ushindi huo muhimu wa magoli 2-3 ambapo Dortmund walikuwa ugenini dhidi ya FC Koln.


Batshuayi amejiunga na klabu hiyo kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu ambapo Dortmund ilimchagua nyota huyo raia wa Ubelgiji kama chaguo sahihi ili kumuachia Pierre Aubameyang aliyejiunga na Arsenyani (Arsenal) na huku Arsenyani wakimruhusu mshambuliaji wake Olivier Giroud kujiunga na Chelsea..

Huu ni mwanzo mzuri kwa nyota huyo katika mchezo wake wa kwanza na kwa maana hiyo anaweza kupata nafasi nzuri katika kikosi hicho ili kurejea vyema kwenye klabu ya Chelsea mwishoni mwa msimu maana atakuwa ameongeza kitu katika kujiamini kwake na hata ubora kuongezeka maana ligi kuu Ujerumani ni moja kati ya ligi ngumu na bora barani Ulaya na hata duniani.

No comments:

Post a Comment