SABABU YA AMPADU KUTUPWA NJE KIKOSI CHA UEFA - Darajani 1905

SABABU YA AMPADU KUTUPWA NJE KIKOSI CHA UEFA

Share This

Nyota wa Chelsea, Ethan Ampadu anatajwa kuachwa kwenye kikosi kitakachoshiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya maarufu kama Uefa Champions League ambapo Chelsea itacheza dhidi ya Barcelona mwezi huu wa Februari.

Nyota huyo aliyejiunga na Chelsea katika dirisha kubwa la usajili la mwaka jana akitokea klabu ya Exeter City amekuwa na kiwango bora klabuni huku akiwa na uwezo mkubwa wa kucheza nafasi za mlinzi wa kati na kama kiungo mkabaji ameachwa katika kikosi cha wachezaji 25 watakaoshiriki michuano hiyo kwa mwaka huu huku ikielezwa sababu ni kutokana na sheria za ligi zinavyosema.

Sheria ya ligi ya mabingwa Ulaya inayomfunga mchezaji huyo ni ile inayosema mchezaji anayeruhusiwa kucheza michuano hiyo awe amezaliwa kuanzia mwaka 1995 mwezi Februari ambapo atakuwa ameichezea klabu yake kwa misimu miwili wakati kwa Ethan Ampadu aliyezaliwa mwaka 1997 mwezi Septemba hajaichezea Chelsea kwa misimu miwili kutokana na kusajiliwa mwaka 2017 lakini kwa kinda mwenzake Callum James Hudson-Odoi ataruhusiwa kucheza na amechaguliwa kwenye kikosi hicho kutokana na kuwa Chelsea toka mwaka 2007.

Lakini Ampadu ataweza kuichezea Chelsea ya vijana kwenye michuano hiyo ya klabu bingwa Ulaya kwa vijana wa akademi ambapo na wao wamefudhu.

Waliochaguliwa; Willy Caballero, Thibaut Courtois, Eduardo, Antonio Rudiger, Marcos Alonso, Davide Zappacosta, Gary Cahill, Andreas Christensen, Cesar Azpilicueta, David Luiz, Emerson Palmieri, Dujon Sterling, Cesc Fabregas, Danny Drinkwater, N'Golo Kante, Ross Barkley, Eden Hazard, Pedro, Tiemoue Bakayoko, Victor Moses, Willian, Kyle Scott*, Alvaro Morata, Olivier Giroud, Callum Hudson-Odoi.

No comments:

Post a Comment