CONTE ATOA NENO KUTAKIWA ITALIA - Darajani 1905

CONTE ATOA NENO KUTAKIWA ITALIA

Share This
Kocha Antonio Conte amefanya mkutano na waandishi wa habari jioni ya leo kuelekea mchezo wa jumatatu ambapo Chelsea itakuwa ugenini kupambana dhidi Watford, kuelekea kwenye mchezo huo hapa nakuletea baadhi ya aliyoyazungumza jioni ya leo.

Waandishi wa habari walimuhoji juu ya kuwepo taarifa kuwa kiongozi wa chama cha soka cha Italia, Costacurta alikuwa njiani kuja kufanya nae mazungumzo juu ya kurejea kuifundisha timu ya taifa ya Italia ambalo ndio taifa la Conte, kocha Antonio Conte alijibu akisema "Costacurta ni rafiki yangu, na tulicheza wote timu ya taifa ya Italia mwaka 1994 lakini kuna kitu nadhani hajakijua ya kwamba mimi bado nina mkataba Chelsea na nauheshimu"

Alipoulizwa kama atakubali kufanya nae mazungumzo ambayo kiongozi huyo mwenye nafasi ya kwekamishna msaidizi wa chama cha soka nchini Italia (FIGC), kocha Antonio Conte alijibu "Kiukweli hapana" alijibu kwa kifupi.

Lakini pia alipoulizwa juu ya hatma yake klabuni Chelsea, kocha Antonio Conte alijibu "Bado nina mkataba hapa na napenda kuendelea kuwa hapa, matamanio yangu niendelee kubaki Chelsea. Hilo ndio muhimu na tarajio langu la kuwa hapa"

Ila pia aliulizwa juu ya kwanini anadhani watu wanasema msimu ujao hatokuwa Chelsea, kocha Antonio Conte alijibu "Sijui kwanini, lakini mimi nina furaha na napenda kubaki hapa zaidi"

Hayo ni baadhi ya aliyoyaongea haswa kuhusu hatma yake klabuni Chelsea akikana kuhusika na kutamani kuondoka klabuni Chelsea

No comments:

Post a Comment