Juzi Chelsea ilikamilisha uhamisho wa nyota raia wa Ufaransa, olivier Giroud ambaye alisajiliwa akitokea klabu ya Arsenyani (Arsenal) ambapo usajili wake uliigharimu Chelsea kiasi cha paundi milioni 18 huku akipewa mkataba wa mwaka mmoja na nusu.
Kumekuwa na maoni tofauti yakitolewa na mashabiki wa Chelsea juu ya usajili huo huku wengi wakilalamika kuwa nyota huyo sio aina ya mchezaji anayehitajika klabuni Chelsea, wengi wakilalamika kuwa nyota huyo ana umri mkubwa kusaini Chelsea ambapo kwa sasa ana miaka 31.
Kocha wa Chelsea ametoa neno juu ya mchezaji huyo ambaye jana alianza mazoezi na klabu, alipoulizwa juu ya nyota huyo kusajiliwa alisema "Giroud ni mchezaji mzuri na ana uzoefu, kumbuka ameshaichezea timu ya taifa ya Ufaransa, kwa hiyo nim mchezaji mwenye uzoefu mkubwa. Niliiambia bodi kuwa nahitaji mchezaji mwenye vigezo kama vyake ndipo na wao wakaniletea huyu. Nafurahia kumpata maana ana sifa nilizokuwa nazihitaji kikosini"
Maneno haya ndio kama iliyoripoti Darajani 1905, muda mfupi mara baada ya Chelsea kumsajili nyota huyo, sisi kama Darajani 1905 tunaamini usajili wa Giroud pale klabuni Chelsea ni kwa kuwa ulihitajika uzoefu zaidi mara baada ya timu kama timu kuona kule kwenye safu ya ushambuliaji kunakosekana mshambuliaji mwenye uzoefu na klabu na ndio maana kocha Conte akamhitaji mchezaji wenye uzoefu huku kigezo cha umri kikiwa sio kigezo muhimu katika usajili huu.
Unapokuwa na washambuliaji wasiokuwa na uzoefu na ligi ngumu kama Uingereza inakuwa ni ngumu kung'aa kwa muda mrefu kisha hapohapo uwe na wachezaji wenye umri mdogo kama Alvaro Morata ambaye hana uzoefu wa kucheza ligi ngumu kama Uingereza alafu amekuwa hatumiki sana kama mshambuliaji namba moja ila mara nyingi amekuwa akitumika kama mshambuliaji mbadala na Michy Batshuayi ametokea Ufaransa na kutua Chelsea ambapo hajatumika sana kwenye michuano mikubwa na hata amekuwa akitumika zaidi kama mbadala wa Diego Costa kwa hiyo hana uzoefu mkubwa wa mikiki ya ligi kuu Uingereza lakini pia kuweza kucheza karibu kila baada ya siku tatu alafu akawa kwenye kiwango chake bora. Kusoma zaidi bonyeza hapa

CONTE ATOA NENO BAADA YA CHELSEA KUMSAJILI GIROUD
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment