Chelsea imekamilisha usajili wa nyota kutoka klabu ya Arsenyani (Arsenal), Olivier Giroud ambaye ametambulishwa rasmi leo na kukabidhiziwa jezi namba 18, ambapo usajili huo unamaanisha nyota huyo anakuja kutoa changamoto mpya kwa mshambuliaji ghali namba moja klabuni Chelsea, Alvaro Morata. Je unamuona Giroud kuwa mtu sahihi kwa Chelsea?
Mimi nawewe wote tutabaki kutoa hisia zetu kama mashabiki lakini naamini kuna faida Chelsea itaenda kufaidika kutoka kwa mchezaji huyo raia wa Ufaransa ingawa wengi wanaupinga usajili huu.
Darajani 1905 bado inaamini Chelsea imemsajili nyota huyu sio kwa malengo ya baadae. Kama alivyokaririwa gwiji wa soka wa zamani wa Chelsea, Frank Lampard pale ambapo Chelsea ilikuwa ikihusishwa kumtaka mshambuliaji wa Stoke city, Peter Crouch, labda nikukumbushe kidogo alisema anamfurahia Peter Crouch kutakiwa na Chelsea kwa maana anamtazama nyota huyo kutua klabuni hapo kama mpango wa muda mfupi ambapo kwa sasa Chelsea haitafuti mshambuliaji atakayetumika kwa miaka mitano au minne huko mbele ila inamsaka mtu mwenye uzoefu na anayeifahamu ligi kuu Uingereza na kuifanya Chelsea ifanikiwe katika malengo yake ya msimu huu.
Ukitaka kukubaliana na hili angalia miaka aliyowekewa Giroud kwenye mkataba wake wa kujiunga na Chelsea, amepewa mkataba wa mwaka mmoja na nusu ambapo hiyo nusu itaisha mwishoni mwa msimu huun na baada ya hapo atakabakiza mwaka mmoja ambapo kwa hapo kama kuna klabu ikivutiwa naye inaweza kumsajili na Chelsea ikapata fungu.
Kutua kwa Giroud klabuni Chelsea kunaweza kuamsha hali mpya kwa mshambuliaji Morata maana ataona kuna mshambuliaji mzoefu na mwenye mikiki anayeifahamu vyema ligi kuu kwa maana hiyo hata Morata ataweza kujifunza vingi kutoka kwa Giroud.
Lakini pia kumbuka Giroud ametua ligi kuu ya Uingereza toka msimu wa 2012/2013, ni misimu mitano mpaka sita sasa toka awepo ligi kuu Uingereza kwa maana hiyo anaweza akawa mwalimu wa Morata kwa maana nyota huyo alifika klabuni bila kukutana na wakongwe wanaocheza nafasi kama yake. Sawa ndio alipata nafasi ya kuzungumza na wakongwe kama Didier Drogba na wengine na wamemweleza mengi kuhusu ligi kuu na mikiki yake lakini inakuwa haileti uhalisia kama angekutana na wakongwe wanaocheza kwa safu yake ambao bado wangekuwepo mpaka sasa. Kama inavyotokea kwa Andreas Christensen kukutana na mtu kama David Luiz kikosini. Morata kuungana na Giroud ni tofauti na Morata alipotua Chelsea na kukutana na Michy Batshuayi.
Nakukumbusha tena kidogo, kocha wa Chelsea, Antonio Conte alipoulizwa juu ya Nemanja Matic kuondoka klabuni Chelsea muda mfupi baada ya Chelsea kumsajili nyota kutoka As Monaco, Bakayoko alisema alikuwa akimtazamia Matic awe mwalimu mzuri kwa Tiemoue Bakayoko kwa maana hiyo Giroud anaweza kuutumia utu uzima wake pale Uingereza kumfundisha mengi Morata na baadae akaja kuwa bora zaidi ya alivyo sasa.

No comments:
Post a Comment