RASMI; GIROUD NI MCHEZAJI WA CHELSEA - Darajani 1905

RASMI; GIROUD NI MCHEZAJI WA CHELSEA

Share This

Kwa sasa tunasema, mchezaji wa zamani wa klabu ya Arsenal, Olivier Giroud amekamilisha uhamisho wa kujiunga na Chelsea rasmi jioni hii kwa  dau linalotajwa kufikia paundi milioni 18.

Nyota huyo raia wa Ufaransa amekamilisha uhamisho huo wa kutua Chelsea muda mfupi mara baada ya nyota wa Chelsea, Michy Batshuayi akionekana akifanyiwa vipimo kwenye klabu ya Borrusia Dortmund ambapo anatajwa kujiunga na klabu hiyo kwa mkopo wa miezi sita huku Giroud akisaini Chelsea kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu ambapo atakuwa mchezaji wa Chelsea mpaka mwishoni mwa msimu ujao.

Lakini pia usajili huo umekamilikia muda mfupi mara baada ya klabu ya zamani ya Arsenyani (Arsenal) kutangaza rasmi kumnasa mshambuliaji wa Borrusia Dortmund, Pierre Aubameyang, ambaye klabu yake imemtumia Michy Batshuayi kama mbadala wa nyota huyo aliyejiunga kwa dau la paundi milioni 55.

Darajani 1905 inaelewa kuwa usajili huu wa Olivier Giroud kutua Chelsea sio usajili wa muda mrefu na ndio maana ata nyota huyo amepatiwa mkataba wa muda mfupi (miezi 18 ambayo ni sawa na mwaka mmoja na miezi sita).

Karibu Stamford Bridge, Olivier Giroud

No comments:

Post a Comment