Maafisa wa serikali ya Urusi wametahadharisha kwamba huwenda nzige wakashambulia viwanja vya mpira wa miguu nchini humo na kuzua kashfa kubwa wakati wa Kombe la Dunia.
Pyotr Chekmarev amesema takriban hektari milioni moja za ardhi kusini mwa Urusi zimevamiwa na wadudu hao.
Volgograd, mji ambao England watachezea dhidi ya Tunisia mnamo 18 Juni, ni moja ya maeneo ambayo yameathiriwa.
Volgograd, mji ambao England watachezea dhidi ya Tunisia mnamo 18 Juni, ni moja ya maeneo ambayo yameathiriwa.
"Tumejifunza kukabiliana na nzige, lakini tutakwepa vipi kutumbukia katika kashfa ya dunia kutokana na nzige mwaka huu?" amesema Chekmarev.
"Ulimwengu wote utafika hapa. Viwanja vya mpira wa miguu vimejaa majani. Nzige hupenda maeneo ambayo kuna majani na rangi ya kijani.
"Utawazuia vipi kufika eneo ambalo mpira unachezewa?" aliongeza Chekmarev, mkuu wa idara ya ukulima katika wizara ya kilimo.
Kombe la Dunia 2018 litaanza mnamo 14 Juni na mechi zitachezewa viwanja 12 katika miji 11 Urusi.
Nyota wa Chelsea, Eden Hazard, Michy Batshuayi na nyota wengine wa Chelsea kama Gary Cahill, Timoue Bakayoko na N'Golo Kante wanaweza wakaikosa michuano hiyo kutokana na kadhaa hiyo ambapomichuano hiyo intarajiwa kufanyika mwaka huu mwezi wa sita. Kama nzige hawa watashambulia itapelekea kuharibu fainali HIZI Basi tutakosa kuwaona mastaa wa Chelsea
Moja ya viwanja vitakavyotumika kwenye fainali za mwaka huu
No comments:
Post a Comment