Klabu ya Torino ya nchini Italia imeanza kulegeza pingu ilizomfunga nyota wake, Andrea Bellotti ambaye aliwai kutakiwa na Chelsea kwa karibu katika dirisha kubwa la usajili lililopita.
Klabu hiyo imekubali kupunguza dau la nyota huyo muitaliano kwa 50% ambapo katika dirisha hilo lililopita klabu hiyo ilihitaji kiasi cha euro milioni 100 ili kumuachia nyota huyo mpaka sasa kuwa tayari kumuuza kwa euro milioni 50.
Dau la nyota huyo limepunguzwa mara baada ya nyota huyo kuonekana kupunguzika ukali wake katika kufumania nyavu kwa msimu huu tofauti na msimu uliopita, na rais wa klabu yake aliwai kutoa tahadhari kwa nyota huyo kuwa kama akiendela na ubutu wake katika ufungaji basi atamuuza kwa bei chee.
Msimu uliopita nyota huyo alicheza michezo 38 huku akifunga magoli 28 wakati kwa msimu huu ameshacheza michezo 25 na amefunga magoli 9 tu mpaka sasa, na ana miaka 24.
No comments:
Post a Comment