Nyota wa Chelsea, Tammy Abraham anayeichezea klabu ya Swansea kwa mkopo amejipanga kufanya makubwa na ana malengo makubwa ya kufanya vizuri ili kujiweka sawa na kuaminika na kupata nafasi kwenye kikosi cha Chelsea msimu ujao.
Tammy ambaye ametokea kwenye akademi ya Chelsea, amejiunga na klabu hiyo ya Swansea katika dirisha kubwa la usajili kwa mkopo huku akiichezea klabu hiyo michezo 32 huku akiifungia magoli 7 amesema anajipanga vyema kupambana katika kipindi hiki kifupi kilichobaki ili aweze kuteuliwa kwenye kikosi kitakachosafiri kuelekea nchini Urusi kwenye kombe la dunia akiwa anaichezea timu ya taifa ya Uingereza na kama hilo litatimia basi atajitahidi kufanya makubwa kwenye nafasi yake ya ushambuliaji ili aweze kurudishwa klabuni Chelsea na kutumika kama mshambuliaji chaguo la kwanza.
Nyota huyo anaamini kurejea kwake Chelsea kutamfanya kupambana zaidi na kuipatia mafanikio klabu yake hiyo iliyomlea mpaka kufikia sasa akiwa kwa mkopo kwenye klabu hiyo ya Swansea.
No comments:
Post a Comment