Daishawin Redan anaipatia ushindi wa muhimu klabu ya Chelsea ya vijana katika mchezo wa ligi kuu Uingereza kwa vijana (Premier League 2) dhidi ya Derby County.
Magoli matatu ya Redan yanaifanya Chelsea kupata ushindi wa tatu kati ya michezo minne ya ligi kuu kwa vijana toka kupoteza kabla ya michezo ya kimataifa ambapo mara baada ya ushindi huo kunaifanya Chelsea ifikie nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Lakini jambo kubwa ukiachana na ushindi ni uwepo wa nyota Ross Barkley ambapo aliichezea timu hiyo ya vijana ili kujiweka sawa kutokana na majeraha yanayomsumbua kwa muda mrefu tangu aliposajiliwa akitokea Everton kwa dau la paundi milioni 15.
Nyota huyo raia wa Uingereza anapambana kujiweka sawa ili kurudi tena kwenye soka la ushindani huku kikwazo alichonacho mpaka sasa ni majeruhi yanayomsumbua.
No comments:
Post a Comment