Klabu ya Chelsea imekumbwa na taarifa mbaya ambapo mchezaji na kocha wa zamani wa klabu hiyo ambaye kwa sasa amekuwa akifanya kazi ya uchambuzi wa soka, Ray Wilkins anatajwa kupatwa na ugonjwa wa mshtuko wa moyo (Cardiac Arrest) na kukimbizwa hospitalini.
Ray Wilkins mwenye miaka 61 aliyewai kuitumikia Chelsea kwa nafasi tofautitofauti kama kocha msaidizi wa Chelsea lakini pia kama mchezaji akicheza nafasi ya kiungo amekumbwa ghafla na ugonjwa huo wa moyo unaosababishwa na moyo kutofanya kazi yake ya kusukuma damu ghafla.
Alikutwa na ugonjwa huo siku ya ijumaa na kukimbizwa hospitali ya St. George ya jijini London.
Kama utakuwa mfuatiliaji mzuri wa Darajani 1905, siku kadhaa zilizopita, gwiji huyo aliwai kuulizwa juu ya nini anakiwaza juu ya mchezo unaokuja wa Chelsea ambapo itakuwa nyumbani kupambana dhidi ya Tottenham, kusoma alichokisema bonyeza hapa
No comments:
Post a Comment