Wakati kaka zao wa Chelsea FC na dada zao wa Chelsea Ladies wakifanikiwa kufudhu kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la FA huko nchini Uingereza, basi wadogo yaani Chelsea youth ambayo ni klabu ya vijana wa chini ya miaka 18 wao walitangazwa kuwa mabingwa wa ligi kuu Uingereza chini ya miaka 18 hapo jana mara baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tottenham hapo jana katika mchezo wa fainali ya ligi hiyo.
Timu hiyo iliyochini ya kocha Jody Morris ilipata magoli yake katika kipindi cha kwanza kupitia kwa nyota wake Charlie Brown ambaye alifunga magoli hayo mawili katika dakika za 18 na dakika ya 45+1' na kuisaidia Chelsea kupata ushindi wake wa 11 ambao ulimaanisha Chelsea inakuwa mabingwa katika taji lake la kwanza msimu huu.
Hongereni vijana..
CHELSEA YATWAA UBINGWA WA LIGI KUU
Share This
Tags
# Chelsea Habari
# Chelsea Youth
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Youth
Labels:
Chelsea Habari,
Chelsea Youth
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment