Mara baada ya kuwa na mapumziko ya mechi za kimataifa kwa upande wa soka la akina dada, Chelsea Ladies jana ilishuka uwanjani kwa mara ya kwanza toka kuisha kwa wiki ya mechi za kimataifa kwa akinadada. Ilishuka uwanjani ili kucheza mchezo wake wa kombe la FA kwa hatua ya robo fainali kama ilivyokuwa kwa kaka zao, Chelsea FC ambao nao jana walikuwa uwanjani kucheza mchezo wa kombe la FA kwa hatua hiyohiyo ya robo fainali.
Na tena kama ilivyokuwa kwa kaka zao ambao walikuwa ugenini kucheza dhidi ya Leicester, basi akinadada, Chelsea Ladies nao walikuwa ugenini kumenyana dhidi ya Liverpool.
Lakini pia kama ilivyo kwa kaka zao wakipata ushindi na kufanikiwa kufudhu kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo, basi akinadada na wao wakafanikiwa kushinda hatua hiyo ya robo fainali kwa kuigaragaza klabu hiyo ya Liverpool Ladies kwa magoli 0-3 na kufanikiwa kufudhu kucheza hatua ya nusu fainali.
Hii ni hatua nzuri kwa klabu zote mbili kuweza kujiweka sawa katika mipango iliyokuwa nayo toka kuanza kwa msimu kwa kupigana katika kila taji au michuano ambayo klabu hizo zinashiriki.
Magoli ya Andersson, Chapman na Mjelde yalitosha kuifanya Chelsea Ladies ifudhu hatua hiyo lakini pia ikiendeleza ubabe wake kwa klabu hiyo ya Liverpool Ladies mara baada ya mchezo uliopita kati ya timu hizo Chelsea kuibamiza klabu hiyo mabao 4-0.
Hongereni dada zetu, Chelsea Ladies
No comments:
Post a Comment