Nyota wa Chelsea, David Luiz anaweza akarejea kwenye mchezo unaofata ambapo Chelsea itakuwa uwanjani kucheza dhidi ya Tottenham siku ya tarehe mosi mwezi Aprili, mchezo wa ligi kuu Uingereza mara baada ya nyota huyo kuwa nje kwa muda mrefu kutokana na majeraha.
Nyota huyo anaweza kurudi kutokana na wasiwasi uliopo juu ya nyota Andreas Christensen ambaye amepata majeraha yaliyomfanya kurudishwa klabuni Chelsea akitokea kwenye timu yake ya taifa, Denmark aliyoungana nayo ili kucheza michezo ya kirafiki.
Lakini kutokana na majeraha yake anaweza akakaa nje kwa muda na kuna wasiwasi akaukosa mchezo huo dhidi ya Tottenham na kueleweka huenda David Luiz akatumika kwenye mchezo huo toka alipocheza kwenye mchezo dhidi ya Watford, mchezo ulioisha kwa Chelsea kupoteza kwa magoli 4-1.
David Luiz alituma picha kwenye mtandao wa Instagram akionekana kuwa sawa kiafya licha ya kuwepo na mfululizo wa taarifa kuwa nyota huyo atakaa nje kwa muda mrefu, na kuna uwezekano akatumika kwenye mchezo huo kama mbadala wa Christensen mwenye miaka 21.
No comments:
Post a Comment