Nyota wa Chelsea, Andreas Christensen amerudishwa klabuni Chelsea akitokea kwenye timu yake ya taifa ya Denmark aliyojiunga nayo ili kucheza michezo ya kirafiki mara baada ya nyota huyo kupata majeruhi.
Kocha wake wa timu ya taifa, Hereide alisema "Tumemrudisha nyumbani, London. Tumeogopa kuwa nae zaidi kutokana na kuogopa kupata madhara zaidi" alisema kocha huyo alipoulizwa juu ya nyota huyo kuachana na timu hiyo ya taifa.
Andreas Christensen mwenye miaka 21 kwa sasa amekuwa akitumika kama chaguo la kwanza kwenye kikosi cha Chelsea amepata majeraha hayo na sasa amerudi klabuni Chelsea ili kufanyiwa matibabu kabla ya mchezo unaofata ambapo Chelsea itakuwa nyumbani kucheza dhidi ya Tottenham siku ya tarehe 1-Aprili.
No comments:
Post a Comment