ISCO AKARIBIA KUTUA CHELSEA - Darajani 1905

ISCO AKARIBIA KUTUA CHELSEA

Share This
Chelsea imekuwa ikitajwa kuifukuzia saini ya nyota raia wa Hispania anayeichezea klabu ya Real Madrid, Isco Alarcon ambaye amekuwa hana uhakika wa kupata nafasi katika kikosi cha kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane.

Isco anadaiwa kuwaambia viongozi wa klabu hiyo kwamba ataondoka klabuni hapo kama akiendelea kutopata nafasi katika klabu hiyo huku akitishia kujiunga na Chelsea ambayo inayomfukuzia lakini pia klabu ya Manchester united. Nyota huyo amekuwa hatumiki kabisa kwenye kikosi cha klabu hiyo huku akipewa nafasi katika michezo 37 klabuni hapo na kwa sasa anatazamia kama ataendelea kukosa nafasi basi ataondoka klabuni hapo.

Iliwai kuripotiwa kuwa Chelsea inaweza kumnasa nyota huyo lakini tu, kama Chelsea itakubali kufanyika kwa mabadilishano ambapo Real Madrid inamtaka Eden Hazard ili nawao wamuachie Isco ili ajiunge na wababe hao.

No comments:

Post a Comment