HAZARD AMPIGIA SIMU WAKALA WAKE, AMWAMBIA ANATAKA KUONDOKA - Darajani 1905

HAZARD AMPIGIA SIMU WAKALA WAKE, AMWAMBIA ANATAKA KUONDOKA

Share This
Mchezo wa Chelsea dhidi ya Manchester city uliochezeka juzi jumapili katika uwanja wa Etihad Stadium ambapo Chelsea ilipoteza mchezo huo kwa kuruhusu goli moja na kushindwa kupata alama yoyote katika mchezo huo, ilicheza chini ya kiwango huku ikionekana dhahiri iliingia ili kujilinda zaidi na sio kutafuta ushindi.

Mara baada ya mchezo huo, nyota wa Chelsea, Eden Hazard alionekana kutokuwa na fraha kabisa kutokana na mchezo aliocheza kuwa nje ya kiwango chake, ba hilo alilikiri kwa kusema ni kweli ilikuwa ngumu kwake kucheza mchezo mzuri kwa maana hakupata nafasi ya kuumiliki mpira. Kama unataka kusoma alichokisema zaidi juu ya mchezo huo, bonyeza hapa

Kutokana na mchezohuo, gwiji wa soka wa zamani, Jamie Carragher ambaye kwa sasa anafanya kazi ya uchambuzi wa soka anaamini mara baada ya mchezo huo, nyota huyo anaweza kudai kuodnoka klabuni hapo. Eden Hazard amekuwa akifukuziwa na vilabu kadhaa barani Ulaya huku Real Madrid wakitajwa kwa aribu kumnunua, jana nilikuletea ripoti juu ya klabu hiyo kumfukuzia na mpaka sasa inatajwa ni jambo moja tu wamebakiza ili kumnasa nyota huyo, kusoma ripoti hiyo, bonyeza hapa

"Mara baada ya mchezo huo, naamini (Hazard) alipokuwa njiani alimpigia wakala wake na kumwambia nitoe klabuni hapa, naamini pia alifadhaika sana mara baada ya mchezo maana anachokiona kwa sasa kutokana na jina lake na ubora wke hajioni kama anacheza kwenye klabu inayotafuta sana mpira, na badala yake anataka kuwa kwenye klabu inayocheza sana mpira na kuumiliki" alisema mchambuzi huyo ambaye kwenye maisha yake ya soka alitamba kwa nafasi ya ulinzi haswa kwenye klabu ya Liverpool.

No comments:

Post a Comment