KUMBE N'GOLO KANTE ALIZIMIA? - Darajani 1905

KUMBE N'GOLO KANTE ALIZIMIA?

Share This

Mchezo wa Chelsea dhidi ya Manchester city ulipoisha huku Chelsea ikipoteza goli 1-0, kocha wa Chelsea alipofanyiwa mahojiano juu ya sababu ya kwanini alipoteza mchezo huo. Conte alisema kutokuwepo kwa Kante pia ilichangia maana amekuwa na umuhimu mkubwa klabuni hapo na hata akileta uwiano sawa. Lakini je umepata kuijua sababu ya kwanini Kante alikosekana? tena taarifa za kukosekana kwake hazikujulikana mpaka pale kikosi kamili cha Chelsea kilipotangazwa, lisaa limoja kabla ya mchezo kuanza.

Je unajua sababu ya kukosekana kwake?

Nyota huyo anayecheza kama kiungo alizimia akiwa mazoezini, siku mbili kabla ya Chelsea kucheza dhidi ya Manchester city ambapo ilihisiwa tatizo la moyo ndio chanzo cha kumfanya azimie ndipo baadae likapatikana wazo la kumpeleka kwa mtaalamu wa magonjwa ya moyo na kufanyiwa vipimo na baadae majibu yakatoka kuwa hana tatizo la moyo na angekuwa tayari kushuka uwanjani kumenyana dhidi ya Manchester city. Na ndio maana alikuwepo kwenye mipango ya kocha na hata hakujumuishwa kwenye orodha ya wagonjwa.

Lakini jumapili asubuhi ambayo ndio ilikuwa siku ya mchezo wenyewe, ndipo kiungo huyo akataarifu kuwa hana hali nzuri, hajisikii vizuri na ndipo kocha Antonio Conte hakutaka kumweka nyota huyo kwenye hatari na hivyo kuamua kutomjumuisha kabisa.

Nyota huyo ameendelea na mazoezi kama kawaida na yupo tayari kupambana dhidi ya Crystal Palace mwisho wa wiki hii katika raundi ya 30 ya ligi kuu Uingereza.

No comments:

Post a Comment