REAL MADRID WABAKISHA KITU KIMOJA KUMNASA HAZARD - Darajani 1905

REAL MADRID WABAKISHA KITU KIMOJA KUMNASA HAZARD

Share This

Eden Hazard mpaka sasa amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na miezi mitatu kuwa kama mchezaji wa Chelsea, na klabu kadhaa barani Ulaya zimekuwa zikivutiwa na kipaji cha nyota huyo na hivyo kumtamani, moja ya klabu hizo, ni klabu kutoka nchini Hispania, Real Madrid ambao wenyewe ndio wanatajwa kumfukuzia mbelgiji huyu kwa karibu huku ikiripotiwa mara kadhaa kuwa kama Chelsea ikishindwa kufudhu kucheza michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa msimu ujao basi itakuwa na nafasi finyu ya kumbakiza nyota huyo aendelee kubaki Stamford Bridge.

Lakini leo pia kuna gazeti limeripoti, ili Eden Hazard abaki klabuni Chelsea basi itategemea juhudi na uhitaji wa klabu ya Real Madrid kuonyesha kwamba inamtaka nyota huyo.

Gazeti hilo limedai kuwa Eden Hazard mwenye miaka 27 amekataa kusaini mkataba mpya klabuni Chelsea ili kusubiri ofa kutoka kwa klabu ya Real Madrid ambapo nyota huyo ataangalia uhitaji na nia ya klabu hiyo kama itahitaji huduma yake.

Lakini pia inaelezwa, nyota huyo ambaye ni mchezaji bora wa nchini Ubelgiji anatakiwa zaidi na kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane na itakuwa ngumu kwake kubaki Chelsea kama Zidane ataendelea kuwa kocha wa Real Madrid maana yeye ndiye anayechochea usajili huo.

No comments:

Post a Comment