EDEN HAZARD ATOA NENO MARA BAADA YA MCHEZO WA JANA - Darajani 1905

EDEN HAZARD ATOA NENO MARA BAADA YA MCHEZO WA JANA

Share This
Mara baada ya Chelsea kupoteza mchezo wake wa jana dhidi ya Manchester city kwa goli 1-0, ambapo Chelsea ilisafiri kuifata klabu hiyo kucheza mchezo huo ambao ulimaanisha Chelsea inatakiwa izidi kupambana ili kujiweka pazuri kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza huku kikubwa kwa sasa kinachoonekana sio kutetea ubingwa wa ligi hiyo ila ni kugombania nafasi nne za juu ili kujihakikishia kucheza ligi ya mabingwa Ulaya smimu ujao.

Mara baada ya mchezo huo, nyota wa Chelsea, Eden Hazard alitoa neno kuhusu mchezo huo na nini anakiona kwa Chelsea ambayo jana haikutumia mfumo au mbinu ya kushamulia ila kutumia mbinu ya kukaba na kujihami sana.

"Tungeweza kucheza kwa masaa matatu, ila nisingeweza kugusa mpira. labda tulicheza vizuri kwa dakika za mwisho ambapo dakika 10 mpaka 15 za mwisho kidogo tulionyesha kumiliki mpira lakini ilitakiwa tufanye hivyo kwa dakika zote za mchezo"

Na alipoulizwa kama anadhani kocha atamtumia tena kama mshambuliaji wa kati, nyota huyo alisema "Sijui, lakini ata kama akinichezesha nafasi hiyo, nitajitoa na kupambana kwa nguvu zangu zote"

"Lakini kiukweli hatujacheza soka zuri kabisa, na hata kwangu inakuwa ngumu kucheza soka safi kwa kugusa mpira mara chache. Nami nililiona pia hilo maana hata tulipokuwa na mpira tulipaswa kutengeneza nafasi na kuzitumia lakini tukafanya makosa. hatukutengeneza nafasi za kutosha" alisema nyota huyo raia wa Ubelgiji.


No comments:

Post a Comment