MORATA ATOA NENO MARA BAADA YA CHELSEA KUPOTEZA DHIDI YA Man City - Darajani 1905

MORATA ATOA NENO MARA BAADA YA CHELSEA KUPOTEZA DHIDI YA Man City

Share This
Nyota wa Chelsea, Alvaro Morata aliingia dakika za jioni katika mchezo wa jana ambapo Chelsea ilipoteza dhidi ya Manchester city katika mchezo wa ligi kuu Uingereza kwa raundi ya 29, na sasa zimebaki raundi 9 ili kumalizika kwa msimu wa 2017-2018 wa ligi hiyo ya nchini Uingereza.

Mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, nyota huyo ametumia mtandao wa Instagram kutuma ujumbe wake kutokana na hali mbaya ya matokeo iliyopo kwa sasa klabuni Chelsea ambapo katika michezo mitano ya mwisho ya ligi kuu, Chelsea imepata ushindi katika mchezo mmoja tu.

"Hiki ndicho kipindi tunahitaji kuwa na umoja kuliko kipindi chochote,hii timu itaendelea kupambana mpaka dakika ya mwisho!! Twendeni pamoja Chelsea" alituma nyota huyo.

Kwa matokeo hayo, Chelsea inashika nafasi ya tano kwa sasa huku ikiwa na alama 53, ikiachwa alama tano na Tottenham inayoshika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu Uingereza huku ikitarajia kucheza mchezo dhidi ya Crystal Palace katika uwanja wa Stamford Bridge siku ya jumamosi.

No comments:

Post a Comment