HERI YA KUZALIWA DANNY DRINKWATER - Darajani 1905

HERI YA KUZALIWA DANNY DRINKWATER

Share This
Leo ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa nyota na kiungo wa Chelsea, Danny Drinkwater akiwa anatimiza miaka 28 toka kuzaliwa kwake mwaka 1990 tarehe 5-Marchi. Nyota huyo ambaye ni raia wa Uingereza lisajiliwa na Chelsea katika dirisha kubwa la  usajili lililopita akitokea klabu ya Leicester, akitua Chelsea kwa dau la paundi milioni 35.

Drinkwater mpaka siku ya njana alikuwa alipocheza mchezo dhidi ya Manchester city, alikuwa akitimiza mchezo wake wa 22 kuichezea Chelsea tangu asajiliwe na wababe hao na mpaka sasa tayari ameshaifungia Chelsea goli moja katika mchewzo dhidi ya Stoke city ambapo Chelsea iliondoka na ushindi mnono wa mabao 5-0.

Jambo ambalo hukuwa ukilijua juu ya nyota huyu alianzia maisha yake ya soka kwa watani wetu mashabiki wa Chelsea, klabu ya Manchester united ingawa hakufanikiwa kuichezea mchezo hata mmoja huku akiishia kutolewa kwa mkopo kabla ya baadae kuuzwa kwenda Leicester hiyo ikiwa mwaka 2012.

No comments:

Post a Comment