GWIJI WA CHELSEA ATAMANI KURUDI TENA - Darajani 1905

GWIJI WA CHELSEA ATAMANI KURUDI TENA

Share This
Chelsea ilikuwa na nyota wengi kutoka barani Amerika, haswa kwenye nchi ya Brazil, mpaka sasa bado wapo akina David Luiz, Willian na hata Kennedy anayecheza kwa mkopo kwenye klabu ya Newcastle. Lakini kuna nyota mmoja kutoka nchini humo aliwai kupita Chelsea na kufanikiwa kushinda mataji yote makubwa akiwa kama kiungo ambaye muda mwengine alikuwa akicheza kama winga wa kulia, Ramires.

Nadhani mashabiki wengi wa Chelsea tunamkumbuka huyu jamaa, haswa tunamkumbuka haswahaswa na lile goli lake alipoifunga Barcelona mwaka 2012 ambapo Chelsea ilikuwa ugenini na ilikuwa ishatanguliwa magoli mawili kabla ya baadae Fernando Torres kuja kufunga goli la mwisho lililoipeleka Chelsea jijini Munich kucheza dhidi ya Bayern Munich katika fainali ya klabu bingwa barani Ulaya kwa mwaka huo.

Sasa nyota huyo mwenye miaka 30 kwa sasa, anatami siku moja kurudi klabuni Chelsea na kucheza tena soka lake la ushindani klabuni hapo, nyota huyo alisema "Chelsea? Mara zote nitabaki kuwa na kumbukumbu za kipekee kucheza soka langu pale, na hata natamani kabla sijastaafu soka langu, siku moja nirudi pale na kuichezea tena"

"Najua milango ya Stamford Bridge ipo wazi muda wote kwa ajili yangu na kama nikifanikiwa kuzivaa jezi zake kwa mara nyengine, litakuwa ni jambo la kuvutia"

"Kumekuwa na tetesi nyingi zikinihusisha na Inter Milan, lakini kiukweli hakuna jambo lolote lakuchochea tetesi hizi zikawa za kweli mpaka sasa. Kila mtu anajua kama Inter ni klabu kubwa barani Ulaya lakini kwa sasa nachokiwaza ni kuisaidia Jiangsu kuwa na mwaka mzuri.Hakuna jambo lolote naloliwaza kwa sasa zaidi ya hilo" alisema nyota huyo aliyeondoka Chelsea mwaka 2016 na kujiunga na klabu ya Jiangsu kwa dau la paundi milioni 25.

No comments:

Post a Comment