CONTE AWAFOKEA WACHAMBUZI, AKUMBUSHIA YA WENGER - Darajani 1905

CONTE AWAFOKEA WACHAMBUZI, AKUMBUSHIA YA WENGER

Share This
Kocha Antonio Conte jana aliiongoza Chelsea kutoka bila alama kwenye jiji la Manchester katika msimu huu mara baada ya kushuhudia Chelsea ikipoteza kwa goli 1-0 dhidi ya Manchester city, lakini wiki iliyopita alitoka kushuhudia Chelsea ikipoteza dhidi ya Manchester united ambao wote wanapatikana kwenye jiji hilo la Manchester. Kwa matokeo haya, Chelsea inakuwa na hali ngumu ya kutusua na kuingia kwenye klabu nne za juu zitakazotakiwa kufudhu na kucheza ligi ya mabingwa msimu ujao maana mpaka sasa Chelsea imeachwa alama tano na klabu inayoshika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu Uingereza.

Mara baada ya mchezo huo kocha Antonio Conte akawajibu wachambuzi waliokosoa mfumo aliotumia wa kujilinda sana dhidi ya Manchester city na kuwaruhusu wamiliki mpira kwa kiasi kikubwa ambapo uchambuzi huo ulitoka kwa wachambuzi maarufu, Jamie Redknapp pamoja na mchezaji wa zamani wa Manchester united, Gary Neville.

Gary Neville ambaye anafanya kazi ya uchambuzi kwa sasa alisema "(Chelsea) walikuwa wakiwaangalia Man city wakicheza. Ilikuwa inauma kuwaangalia, haswa kwa heshima ya ligi kuu Uingereza, ilikuwa ni uzalilishaji" wakati Redknapp alisema "walishakubali kupoteza alama tatu ata kabla ya mchezo kuanza"

Kocha Antonio Conte aliwajibu kwa kusma "Nisingeweza kukubali kushuhudia tunafungwa magoli 3-0 au 4-0, ukiangalia muda kidogo umepita toka Manchester city walipomenyana dhidi ya Arsenal, na wachambuzi haohao walimlalamikia Wenger kwa kuiruhusu Man city kupata magoli matatu ndani ya dakika 30"

"Wachambuzi inabidi watumie vichwa vyao vizuri katika kutafsiri juu ya mifumo na aina ya uchezaji maana naamini wana ufahamu na sio kuongea kama wajinga" alisema kocha huyo raia wa Italia.


No comments:

Post a Comment