CESAR AZPILICUETA ATUMA UJUMBE MZITO - Darajani 1905

CESAR AZPILICUETA ATUMA UJUMBE MZITO

Share This
Chelsea imepoteza mchezo wake wa muhimu dhidi ya Manchester city hapo jana kwa goli 1-0 ambapo Chelsea ilihitaji ipate ushindi katika mchezo huo ili ijiweke katika nafasi nzuri ya kuwania kucheza michuano ya klabu bingwa barani Ulaya msimu ujao.

Kutokana na matokeo hayo, Chelsea inakuwa imeachwa alama tano na Tottenham inayoshika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu Uingereza ikiwa na alama 58 wakati Chelsea inashika nafasi ya tano ikiwa na alama 53, nafasi ambayo kama mpaka msimu ukiisha ikiendelea kuwa hapo basi itamaanisha haitofanikiwa kufudhu kucheza michuano hiyo ya klabu bingwa msimu ujao.

Kutokana na matokeo hayo, nahodha msaidizi wa Chelsea, Cesar Azpilicueta ametuma ujumbe katika mtandao wa Twitter kuonyesha kuhuzunika kwake na matokeo hayo yaliyotokea jana katika mchezo dhidi ya Manchester city.

"Kuonyesha ni kwa kiasi gani tumeumizwa na matokeo haya itakuwa ni ngumu kuyaelezea katika maneno. Asanteni mashabiki wote duniani kwa kutuonyesha ushirikiano wenu" alituma ujumbe huo mlinzi huyo raia wa Hispania.

No comments:

Post a Comment