PL; FT, Man city 1-0 CHELSEA - Darajani 1905

PL; FT, Man city 1-0 CHELSEA

Share This

Chelsea inapoteza mchezo wake wa pili katika jiji la Manchester mara baada ya kupoteza mchezo wake wa raundi ya 29 dhidi ya Manchester city kwa goli 1-0, goli likifungwa dakika ya 46 na Bernardo Silva.

Chelsea ilianza mchezo kwa kujilinda zaidi na kufanya mashambulizi ya kushtukiza ambapo mpaka kipindi cha kwanza kinaisha ilikuwa na umiliki wa mpira kwa uwiano mdogo huku kipindi iko kikiisha kwa suluhu. Mpaka wapinzani hao wakija kupata goli kipindi cha pili.

Ingawa Chelsea iliingia na mpango wa kujilinda zaidi huku ikitumia mashambulizi ya kushtukiza, lakini haikuwa makini katika mashambulizi hayo ikikosa maelewano katika nafasi walizozipata ambapo maelewano kati ya washambuliaji wake yalikosekana na hivyo mashambulizi kuishia kwa walinzi na kipa wa Manchester city.

Lakini Chelsea imeonyesha soka safi licha ya kucheza bila nyota wake N'golo Kante aliyekuwa nje kutokana na kutokuwa sawa kiafya, ambapo kuumwa kwake kumetaarifiwa muda mfupi kabla ya mchezo huo.

Kwa matokeo haya yanaifanya Chelsea iachwe alama 5 na aliyejuu yake ambaye ni Tottenham ambao jana walipata ushindi na kuifanya ikae katika nafasi nne za juu.

No comments:

Post a Comment