Chelsea inajiandaa kushuka uwanjani keshokutwa kucheza mchezo wake wa klabu bingwa barani Ulaya ambapo itakuwa uwanjani kumenyana dhidi ya Barcelona kwenye uwanja wa Camp Nou uko nchini Hispania.
Kuelekea kwenye mchezo huo ambao Chelsea itahitaji sare yoyote ya magoli kuanzia 2-2 na kuendelea au kupata ushindi wowote ili kufanikiwa kufudhu katika michuano hiyo kwa hatua ya robo fainali, kocha Antonio Conte ametoa neno akiwa mazoezini na timu hiyo ambapo amekuja na mpango kabambe ili kuikabili timu hiyo katika mchezo huo. Kupitia mtandao wa klabu hiyo, kocha huyo ameeleza mpango kabambe huo aliokuja nao kabla ya klabu hiyo kusafiri mpaka nchini Hispania kumenyana dhidi ya wababe hao.
"Kwa sasa inatakiwa tujiandae vyema kwa ajili ya mchezo huo, nadhani muda mwengine inabidi utoe ushirikiano na wengine ili kutimiza majukumu, nami nimeamua kufanya hivyo na wachezaji wangu ambao wao ndio watakuwa uwanjani kucheza mchezo huo"
"Ni kweli, kwa kila mchezo natakiwa kuchagua kikosi cha wachezaji 11 kwa kuwa wachezaji ni wachezaji na wao wana majukumu yao, nami kocha ni kocha na nina majukumu yangu. Lakini muda mwengine kwa michezo kama hii unatakiwa kama kocha uwahusishe zaidi wachezaji na uwasikilize nini wanaona kinafaa kukifanya. Kwa maana pia mchezo wenyewe upo karibu sana na inatakiwa tuwe na mpango madhubuti katika kipindi hiki kifupi ili kuweza kuwakabili"
"Tuna mchezo muhimu, hautokuwa rahisi, lakini tunatakiwa kujaribu kupambana na kuweza kuwakabili. Kuwapa wapinzani wenu muda mwingi wa kumiliki mpira, haswa katika ardhi ya nyumbani kwao ambapo hiyo itataikiwa twende nayo sawa kwa kuonyesha ukomavu na kiasi gani tunajari mchezo huo na kujitahidi kusubiri pale tunapopata nafasi ili tuzitumie vizuri"
"Inatakiwa tuwe vizuri, lakini unapocheza na timu za aina hii, ambazo nadhani ni moja kati ya timu bora duniani, inatakiwa ujiandae kupambana sana kama ilivyotokea katika mchezo wa kwanza ambapo nadhani tulikuwa zaidi ya bora. Hii (Chelsea) sio timu yenye udhoefu mkubwa katika michuano hii, tuna wachezaji ambao ndio kwanza wanashiriki michuano hii katika msimu wao wa kwanza, wengine wa pili, lakini tunatakiwa kupambana kufanya kazi kama timu na kuwa tayari kupamabana na kwa muda wote kuwa tayari kufunga pale tunapopata nafasi" alisema kocha huyo.
Katika mchezo wa kwanza uliochezwa tarehe 20-Februari baina ya timu
hizo, uliisha kwa suluhu y1 1-1 katika uwanja wa Stamford Bridge ambapo
Chelsea ilikuwa nyumbani.
KOCHA CONTE AELEZA MPANGO WAKE ATAKAOTUMIA DHIDI YA Barcelona
Share This
Tags
# Chelsea FC
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea FC,
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment