Nyota wa Chelsea aliyejiunga kwa mkopo klabu ya Sunderland, Jake Clarke-Salter jana aliiongoza vyema timu yake ya taifa ya Uingereza chini ya miaka 21 kuibamiza timu ya taifa ya Romania ya chini ya miaka 21 kwa magoli 2-1 huku nyota huyo ambaye anacheza nafasi ya mlinzi wa kati.
Goli lake alilofunga kwa kichwa dakika ya 73 liliifanya timu yake ya Uingereza iwe mbele kwa magoli 2-0 kabla ya mchezaji wa Romania kuchomoa goli moja na kufanya matokeo kuwa 2-1 mpaka kumalizika kwa mchezo huo wa kirafiki.
Clarke-Salter aliyeiongoza timu ya taifa ya nchi hiyo ya Uingereza kuwa mabingwa wa kombe la dunia mwaka 2017 ya chini ya miaka 20, ameifungia goli hilo muhimu timu hiyo likiwa ni goli lake la kwanza kwa timu hiyo ya chini ya miaka 21 huku akicheza nafasi ya ulinzi wa kati, sambamba na nyota mwenzake wa Chelsea anayeichezea Hull city kwa mkopo, Fikoyi Tomori.
No comments:
Post a Comment