Chelsea kwa sasa ipo mapumzikoni, kutokana na kupisha michezo ya kirafiki ya timu za taifa, ratiba inayotambulika na chama cha soka duniani maarufu kama FIFA. Kuna wachezaji ambao walichaguliwa na timu zao za taifa kwa sasa wapo huko kutumikia majukumu yao katika mataifa yao, lakini mmoja wa nyota walioitwa ni mlinda mlango nambari moja wa Chelsea, Thibaut Courtois. Ambaye aliungana na timu yake ya taifa ya Ubelgiji.
Mlinda mlango huyo anatajwa kuachana na timu yake ya taifa na kwa sasa amerejea nchini Uingereza kuungana na Chelsea kutokana na majeraha aliyokuwa nayo.
Taarifa zinadai kuwa Courtois alijiunga na timu yake ya taifa akiwa na majeraha aliyokuwa nayo tangu kabla ya mchezo wa Chelsea dhidi ya Leicester na sasa anatajwa kulazimishwa na makocha wa timu yake hiyo ya taifa kurejea Chelsea mara baada ya kufanya mazoezi ya peke yake akiwa kwenye timu hiyo ya taifa kutokana na majeraha aliyokuwa nayo.
Thibaut Courtois anaungana na nyota kama Andreas Christensen, na Ethan Ampadu ambao wote wamerejea Chelsea kutoka kwenye timu zao za taifa kutokana na majeraha huku Chelsea ikiwa na mchezo mgumu dhidi ya Tottenham.
No comments:
Post a Comment