UEFA wamfungia mlango Batshuayi - Darajani 1905

UEFA wamfungia mlango Batshuayi

Share This

Tarehe 22-Februari klabu ya Borrusia Dortmund ya nchini Ujerumani ilikuwa uwanjani nchini Italia kumenyana dhidi ya Atalanta katika ligi ya Europa, ulikuwa ni mchezo wa marudiano mara baada ya mchezo wa kwanza kuisha kwa Dortmund kushinda 3-2 na sasa walikuwa nchini Italia ili kucheza mchezo wa marudiano.

Mchezo huo ukachezeka na kuisha kwa matokeo ya 1-1 na kuifanya Dortmund ifudhu kucheza hatua inayofata. Lakini gumzo mara baada ya mchezo huo liliiburiwa na nyota wa Chelsea, Michy Batshuayi anayeichezea Dortmund kwa mkopo wa miezi sita mara baada ya kutoa malalamiko kwa mashabiki wa klabu hiyo ambao anadai walikuwa wakiimba nyimbo za kibaguzi wa rangi kwa nyota huyo.

Mara baada ya malalamiko hayo chama cha soka barani Ulaya maarufu kama UEFA wakadai wapo tayari kufanya uchunguzi juu ya shutma izo na kuahidi kuadhibiwa kwa klabu hiyo kama ikigundulika ni kweli ubaguzi huo ulifanyika. Lakini sasa kumetoka taarifa mpya juu ya chama hicho cha soka zikidai kuwa chama hicho cha soka kimekataa kuendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo na kuna uwezekano kwa klabu hiyo kutoadhibiwa.

Hii sio mara ya kwanza kwa klabu ya Atalanta kushutumiwa juu ya tabia yake ya kujihusisha na ubaguzi wa rangi.

No comments:

Post a Comment