Chelsea imepoteza alama muhimu katika mchezo wa jana mara baada ya kupata alama moja kati ya tatu ilizopaswa izipate kama ingefanikiwa kupata ushindi katika mchezo huo dhidi ya West Ham ambapo mchezo uliisha kwa sare ya 1-1 huku goli la Chelsea likifungwa na mlinzi Cesar Azpilicueta ambaye alifunga katika kipindi cha kwanza dakika ya 36.
Mara baada ya mchezo huo, mbio za kugombania nafasi ya kucheza michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa msimu ujao ni kama zimefifia kwa upande wa Chelsea kutokana na kuachwa kwa pengo la alama kumi na Tottenham inayoshika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza.
"Kwa sasa tupo mbali kuliko kipindi chochote. Kombe la FA ni taji kubwa na muhimu likiwa na historia kubwa lakini kwetu halitoshi. Tutajaribu kupambana kulitwaa ila halitofanya msimu kuwa mzuri kwetu" alisema nahodha msaidizi wa Chelsea, Cesar Azpilicueta.
Chelsea imebakisha matumaini ya kutwaa taji moja msimu huu, taji la kombe la FA ikiwa kwenye hatua ya nusu fainali ambapo itacheza dhidi ya Southampton uku ikishindwa kulitetea taji lake la ligi kuu Uingereza ililoshinda msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment