Klabu ya Chelsea inatajwa kumfukuzia nyota raia wa Ivory Coast anayeichezea klabu ya OGC Nice ya nchini Ufaransa, Jean Michael-Seri.
Hiyo ni kama ilivyoripotiwa na gazeti la nchini Ufaransa, gazeti L'Equipe ambalo limedai Chelsea inaweza kumsajili nyota huyo anayetajwa kuwa na thamani ya paundi milioni 40 mara baada ya klabu pinzani kwenye usajili huo, klabu ya Barcelona kuamua kuachana na mpango wa kumsajili kiungo huyo mwenye urefu wa futi 5.
Jean Michael Seri amekuwa akitakiwa na Chelsea iliyokuwa ikichuana na Barcelona kwa muda sasa huku nyota huyo akikiri anahitaji kuachana na klabu hiyo ya nchini Ufaransa na anahitaji kupata changamoto nyengine kutoka kwenye klabu nyengine. Lakini gazeti hilo linaripoti kuwa klabu za Manchester city na Manchester unired nazo zimeingia kwenye mpango wa kumnasa nyota huyo mwenye miaka 26.
No comments:
Post a Comment