Habari muhimu kuelekea Chelsea vs Tottenham - Darajani 1905

Habari muhimu kuelekea Chelsea vs Tottenham

Share This

Chelsea itakuwa nyumbani jioni ya leo ili kucheza mchezo wake wa 31 wa ligi kuu Uingereza dhidi ya Tottenham Hotspurs, mchezo unaowataka Chelsa ipate ushindi ili kujiweka vyema kwenye harakati zake za kugombea nafasi nne za juu katika msimamo wa ligi kuu Uingereza ambapo kama watafanikiwa kuingia kwenye nafasi hizo basi itawafanya wafudhu kucheza michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.

Kuelekea kwenye mchezo huo, hapa nakuletea habari muhimu na matukio yote unayopaswa kuyafahamu au kuyajua kuelekea mchezo huo wa watani wa jadi kutokea London.

Habari muhimu;
Chelsea; Huu ni mchezo ambao ni lazima Chelsea ihakikishe inapata ushindi na kuondoka na alama zote tatu. Lakini wachezaji ambao inaonekana wataukosa mchezo huo ni pamoja na Ethan Ampadu ambaye alipata majeraha akiwa anaiongoza klabu ya vijana ya Chelsea kucheza mchezo wake wa ligi ya mabingwa dhidi ya Real Madrid. Andreas Christensen, haikutimikia timu yake ya taifa ya Denmark kutokana na majeraha na hivyo kurudishwa London ili apambane na majeraha hayo akiwa na klabu yake.

Thibaut Courtois naye pia alirudishwa na timu yake ya taifa ya Ubelgiji ili aje ajiweke sawa kiafya kutokana na majeraha aliyoyapata ata kabla ya mchezo wa kombe la FA ambapo Chelsea ilishinda ugenini kwa magoli 1-2 dhidi ya Leicester city. Ross Barkley naye ataukosa mchezo wa leo licha ya jana kuitumikia klabu ya vijana ya Chelsea ilipomenyana dhidi ya klabu ya vijana ya Derby County. David Luiz nae ataukosa mchezo wa leo na hivyo kuonekana Gary Cahill kuweza kutumika kama mlinzi wa kati.

Tottenham; Klabu hii iliyochini ya kocha Mauricio Pochettino itashuka uwanjani ikiwa haina mchezaji yoyote majeruhi ingawa mshambuliaji wake Harry Kane anaweza kuukosa mchezo huu.

Mwamuzi; Adre Marriner ndiye mwamuzi wa mchezo wa leo na mpaka sasa amekuwa mwamuzi kwenye michezo 21 ya ligi kuu huku akitoa kadi za njano 54 na kadi nyekundu 2.

Rekodi; Chelsea ikiwa nyumbani Stamford Bridge ina rekodi nzito dhidi ya klabu hiyo ya Tottenham ambapo toka mwaka 1990 mpaka leo haijawai kupoteza mchezo wowote.

Michezo iliyopita;
Chelsea: LLWLW
Tottenham: WWLWW

Muda; Saa 6:00 Usiku (Saa 18:00) kwa saa za Afrika Mashariki

No comments:

Post a Comment