Tarehe 10-Aprili-1996, familia ya mzee Sten Christensen ilibarikiwa kupata mtoto wa kiume aliyepewa jina la Andreas Christensen ambaye leo anatajwa kuwa mmoja wa walinzi bora mwenye umri mdogo.
Nyota huyo leo anatimiza miaka 22 huku akiwa muhimili mkubwa kwenye safu ya ulinzi ya Chelsea chini ya kocha Antonio Conte.
Alianza maisha yake ya soka akiwa kwenye klabu ya Brøndby IF ya uko nchini Denmark, klabu aliyokuwa anaichezea baba yake mzee Sten Christensen, hiyo ilikuwa mwaka 2004 akiwa na miaka 8 mpaka alipoachana na klabu hiyo mwaka 2012.
Mwaka 2013 mara baada ya kufukuziwa na klabu nyingi barani Ulaya, klabu kama Arsenal, Manchester city na Bayern Munich huku Chelsea ikiwemo, hatimaye akaamua kusaini klabuni Chelsea, hiyo ilikuwa mwaka 2013. Lakini baadae akatolewa kwa mkopo na kujiunga na klabu ya nchini Ujerumani, Borrusia Monchnglebach ambapo huko alicheza kwa mafanikio makubwa mpaka kumshawishi kocha wa Chelsea kwa mwaka 2017, Antonio Conte kuliorodhesha jina lake akimhitaji arejee Chelsea.
Na ndio mpaka sasa yupo Chelsea huku akitajwa kuwa mrithi sahihi wa mchezaji wa zamani wa Chelsea, John Terry.
Heri ya kuzaliwa Andreas Christensen..
No comments:
Post a Comment